Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico ameandika barua ya kujiuzulu kwenda kwa Rais wa nchi hiyo, baada ya kutokea mauaji ya mwandishi wa habari Jan Kuciak na mpenzi wake Martin Kusnirova.
Rais wa taifa hilo, Andrej Kiska amekubaliana na uamuzi huo wa Waziri Mkuu na kumuagiza Naibu Waziri Mkuu, Peter Pellegrin kuunda Serikali mpya.
Aidha, kwa takribani wiki mbili wananchi wamekuwa wakiandamana kupinga mauaji ya mwanahabari huyo aliyebobea katika kuandika habari za kiuchunguzi.
Hata hivyo, Robert Fico ametumikia nafasi hiyo ya Waziri Mkuu wa Slovakia kwa miaka 10 amelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya chama kimoja cha upinzani kilichoshiriki kuunda Serikali kutangaza nia ya kujitoa katika Serikali ya nchi hiyo.