Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif amekanusha madai kwamba alihusika na jaribio la mauaji ya kiongozi wa upinzani Imran Khan, mnamo wakati wafuasi wa waziri mkuu huyo wa zamani wakiendelea kuandamana, wakitaka uchunguzi wa tukio hilo.

Khan alipigwa risasi mguuni wakati wa mandamano ya kupinga serikali siku ya Alhamisi. Mcheza Kriketi huyo aliyegeuka mwanasiasa amemlaumu waziri mkuu Sharif, waziri wa mambo ya ndani Rana Sanaullah na jenerali wa juu wa jeshi la Pakistan kwa kujaribu kumuua.

Kiongozi wa upinzani na Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan. Picha ya Tribune India.

Sharif amesema jana Jumamosi kwamba waziri mkuu huyo wa zamani alikuwa anaharibu nchi kwa kutoa madai ya uongo na kuongeza kwamba hakukuwa na ushahidi dhidi ya watu watatu wanaolaumiwa na Khan na kuitaka mahakama ya juu kuunda tume ya mahakama kuchunguza madai hayo aliyoyataja kuwa mazito.

Novemba 3, 2022, Vyombo mbalimbali vya Hbari viliripoti tukio la Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan kunusurika kifo baada ya msafara wake kushambuliwa kwa bunduki alipokuwa akifanya maandamano katika mji wa Wazirabad mashariki mwa nchi na alijeruhiwa mguuni kwa risasi.

Ajali ya ndege Bukoba: Manusura wapelekwa Hospitali
Ajali ya Ndege Bukoba: juhudi za uokoaji zinaendelea