Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhakikisha anasimamia mifuko ya maendeleo iliyoanzishwa na serikali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kwa tija.
Ameyasema hayo leo Novemba 13, 2020 katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la 12 Jijini Dodoma.
Aidha amemuagiza Waziri Mkuu kuangalia uwezekano wa kuunganisha baadhi ya mifuko hiyo ili kupunguza gharama za uendeshaji na kusaidia kufanya kazi kwa tija hasa kwa wananchi wa kawaida wakiwemo wamachinga, mama lishe na wajasiriamali wadogo.
Baadhi ya mifuko hiyo ni mfuko wa maendeleo ya vijana, mfuko wa maendeleo ya wanawake, mfuko wa taifa wakuendelezea wajasiriamali, mfuko wa kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo na mfuko wa kilimo