Polisi nchini Japan, inamshikilia mwanamume mmoja (40), kwa tuhuma za kuhusika na jaribio la kumuua Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe kwa kupigwa risasi akiwa kwenye hafla ya kampeni eneo la Nara nchini humo.
Kiongozi huyo wa zamani alikuwa akitoa hotuba katika hafla ya kuelekea uchaguzi wa baraza la juu Juni 3, 2022 wakati milio dhahiri ya risasi iliposikika na kumpata.
“Alikuwa akitoa hotuba na mwanamume akatokea nyuma, risasi ya kwanza ilisikika kama ni bandia na hakuanguka na kulikuwa na kishindo kikubwa, lakini baada ya risasi ya pili, watu walimzunguka na kuona ni kweli hivyo kuanza kumpa massage ya moyo, unaweza kuona cheche na moshi,” msichana mmoja alishuhudia akiwa eneo la tukio.
Shizo Abe (67), alianguka na alikuwa akivuja damu shingoni, na alipata msaada kutoka kwa Viongozi na wanachama wa chama tawala cha Liberal Democratic Party ingawa LDP na Polisi wa eneo hilo hawakuweza kuthibitisha ripoti hizo mara moja.
Hata hivyo, Waziri huyo mstaafu alipelekwa hospitalini na alionekana kuwa katika hali ya kukamatwa kwa moyo na kushindwa kupumua neno ambalo linatumiwa nchini Japani likionesha kutokuwepo kwa dalili muhimu, na kwa ujumla kabla ya kuthibitishwa rasmi kwa kifo na Daktari.
Kufuatioa shambulio hilo, Serikali imesema tayari kikosi kazi kimeundwa kufuatilia tukio hilo na kwamba Msemaji Mkuu wa Serikali anatarajiwa kuzungumza hivi karibuni baada ya kupatikana kwa taarifa za kiuchunguzi.
Abe, waziri mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi nchini Japan, alishika wadhifa huo mwaka 2006 kwa mwaka mmoja na pia kuanza tena wadhifa huo 2012 hadi 2020 hadi alipolazimika kuachia ngazi kutokana na ugonjwa wa kudhoofika kwa utumbo mpana.
Inaarifiwa kuwa, Japani ina baadhi ya sheria kali zaidi za kudhibiti bunduki Duniani, na vifo vya kila mwaka kutokana na bunduki katika nchi hiyo yenye watu milioni 125 mara kwa mara huwa katika takwimu moja na mchakato wa kupata leseni ya bunduki ni mrefu na mgumu unaothibitishwana chama cha ufyatuaji risasi kabla ya kukaguliwa na polisi.