Waziri mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane ametangaza kujiuzulu baada ya kuhusishwa na mauaji ya mke wake wa zamani Lipolelo Thabane.
Aliyekuwa mke wake Lipolelo aliuawa baada ya kupigwa risasi nje ya nyumba yake siku mbili kabla ya Thabane kuapishwa kama Waziri Mkuu wa Lesotho.
Aidha Thabane (80) hajasema ni lini ataondoka rasmi ofisini lakini Chama chake cha All Basotho Convention (ABC) kimesema kiongozi mpya ataapishwa Jumatano.
Hata hivyo Mke wa sasa wa Thabane, Maesaiah Thabane (43) ameshtakiwa kwa mauaji ya Lipolelo Februari mwaka huu na yupo nje kwa dhamana, ambapo Wawili hao wote wamekana kuhusika na mauaji hayo.