Waziri Mkuu wa serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa Fayez Serraj ametangaza nia ya kukabidhi madaraka kwa uongozi mpya mwezi Oktoba, wakati mazungumzo ya kusuluhisha mzozo nchini humo yakiendelea.
Serraj amesema kuwa majadiliano ya hivi karibuni baina ya pande hasimu ambayo yalidhaminiwa na Umoja wa Mataifa, yameifikisha Libya katika kipindi kipya cha maandalizi ya kuziunganisha taasisi za kitaifa, na kusafisha njia kuelekea uchaguzi wa Bunge na Rais.
”Natangaza nia yangu ya dhati ya kukabidhi hatamu za uongozi kwa baraza la utawala linalofuata, kabla ya mwezi Oktoba kumalizika,” amesema Fayez.
Aidha, Fayez Serraj amesema kuwa ni katika mazingira hayo ya kuelekea uchaguzi, ambapo ananuia kuachia ngazi.