Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe amefariki dunia baada ya kupigwa risasi wakati akihutubia kwenye kampeni za uchaguzi wa ubunge katika mji wa Nara nchini humo.

Abe (67) alipigwa risasi mara mbili ambapo moja ilimpata kifuani na nyingine mgongoni ambayo ilisababisha aanguke chini na kukimbizwa Hospitalini kwa msaada wa Viongozi na wanachama wa chama tawala cha Liberal Democratic Party ingawa LDP.

Waziri Mkuu wa sasa wa nchi hiyo, Fumio Kishida amesema hali ya Abe ilibadilika ghafla wakati akipatiwa matibabu na kwamba tayari mtuhumiwa wa tukio hilo amekamatwa na Polisi.

Shinzo Abe (67)

Serikali imesema, tayari kikosi kazi kimeundwa kufuatilia tukio hilo na kwamba Msemaji Mkuu wa Serikali anatarajiwa kuzungumza hivi karibuni baada ya kupatikana kwa taarifa za kiuchunguzi.

Abe, waziri mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi nchini Japan, alishika wadhifa huo mwaka 2006 kwa mwaka mmoja na pia kuanza tena wadhifa huo 2012 hadi 2020 hadi alipolazimika kuachia ngazi kutokana na ugonjwa wa kudhoofika kwa utumbo mpana.

Inaarifiwa kuwa, Japani ina baadhi ya sheria kali zaidi za kudhibiti bunduki Duniani, na vifo vya kila mwaka kutokana na bunduki katika nchi hiyo yenye watu milioni 125 mara kwa mara huwa katika takwimu moja na mchakato wa kupata leseni ya bunduki ni mrefu na mgumu unaothibitishwana chama cha ufyatuaji risasi kabla ya kukaguliwa na polisi.

Shinzo Abe (67)

Kiongozi CCM afariki ghalfa Msikitini
Kina Mdee wapeta Mahakama Kuu, waruhusiwa kupinga 'ya CHADEMA'