Rais wa Senegal Macky Sall, amemsimamisha kazi Waziri wa Afya wa nchi hiyo Abdoulaye Diouf Sarr, baada ya tukio la watoto wachanga 11 kuuawa na moto katika chumba cha hospitali ya watoto wachanga.

Rais Sall, kupitia ukurasa wake wa Twitter ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya vichanga hao.

Nafasi ya Sarr inachukuliwa na Marie Khemesse Ngom Ndiaye, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, kwa mujibu wa amri ya serikali.

Meya wa mji wa Tivaouane Demba Diop amesema moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme na ulisambaa kwa haraka sana.

Kwa mujibu wa Maafisa wamesema kuwa hitilafu ya umeme ndio ilisababisha moto kuzuka Jumatano jioni na kuua watoto hao wachanga katika hospitali ya mji wa magharibi mwa Senegal wa Tivaouane.

Pablo: Utakua mchezo mgumu, tumejiandaa kushinda
Watoto wafariki kwa kunywa sumu