Waziri Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amefungua kikao cha Pili cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kikao hicho kimeendeshwa kwa mara ya kwanza kwa njia ya mtandao (zoom) ambapo Wziri alifungua kikao kutokea ofisini kwake Mtumba Mkoani Dodoma na wajumbe wakiwa Morogoro.
Agenda za kikao hicho ni kupitia Taarifa ya Mpango wa utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Mwelekeo wa Bajeti ya mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na dondoo kutoka kwa wajumbe.
Taarifa hiyo iliwasilishwa mbele ya Baraza na Kaimu Kamishna wa Sera na Mipango Alexander Allen Temu, ambapo wajumbe walipata fursa ya kuijadili kwa kina na kutoa mapendekezo yao ambapo Mwenyekiti ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Muasilishaji mada walitoa majibu ya hoja zilizoibuliwa na wajumbe.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Dkt. Stergomena aliwakumbusha wajumbe wa Baraza kuwa lengo la kuanzishwa kwa mabaraza ya wafanyakazi.
“Kama tunavyofahamu lengo la kuanzishwa kwa mabaraza ya wafanyakazi mahali pa kazi ni kuimarisha utendaji kazi wa pamoja kati ya waajiri na wafanyakazi”, Amesema Waziri Tax
“Shughuli mbalimbali zilizotekelezwa, baadhi ya shughli zilizotekelezwa ni pamoja na kulipa madeni mbalimbali ya wazabuni, kufanya tafiti, kulipa mishahara kwa wanajeshi, watumishi wa umma kwa wakati kulingana na stahili zao, kulipa posho ya chakula kwa Maafisa, askari na vijana wa JKT kufuatilia misamaha ya kodi na ushuru wa bidhaa, kuendelea kutoa ushauri kwenye miradi ya ujenzi kwa Wizara na taasisi zingine, kufanikisha sherehe mbalimbali na maadhimisho ya kijeshi ya kitaifa, kutatua mogoro ya ardhi kwa kupima, kufanya tathimini na kulipa fidia kwa bbadhi ya maeneo”
Aidha, Dkt Stergomena alitoa pongezi kwa wajumbe kwa kufanikisha utekelezaji wa majukumu hayo na Serikali kwa kutoa kipaumbele kwa sekta ya ulinzi.
Dkt. Stergomena ametoa wito na kuwaomba wajumbe kusimamia na kuwahimiza watumishi kufanya kazi kwa weledi, kwa uadilifu na kuepuka ubadhilifu wa rasilimali za Taifa na kujilinda dhidhi ya magonjwa ambukizi nay ale yasiyoambukiza.
“ napenda kuwasistiza na kuwaomba wajumbe kuwa wasimamizi wa mambo manne ambayo nitayataja hapa na kuahimiza watumishi kuyazingatia. Jambo la kwanza ni kufanya kazi kwa weledi, kufanya kazi kwa udilifu pamoaja na uadilifu kazini, kulinda rasilimali za taifa letu pamoja na kujilinda na magonjwa hatari yakiwemo UKIMWI na UVIKO – 19 na magonjwa mengine yasiyoambiza”, amesisitiza
Vikao vya mabaraza ya wafanyakazi ni utekelezaji wa takwa la kisheria ambalo chimbuko lake ni Tamko la Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere (Tamko Na. 1 la Mwaka 1970) na Sheria nyingine za kazi za nchi yetu na zile za kimataifa zinazohimiza ushirikishwaji wa wafanyakazi katika kufanya maamuzi mbalimbali kupitia mabaraza ya wafanyakazi. Aidha, Baraza hili ni jukwaa muhimu sana mahali pa kazi kwani ni kiungo kati ya Menejimenti na Wafanyakazi.