Macho na masikio ya wafanyakazi wa umma na sekta binafsi yataelekezwa leo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mgeni rasmi sherehe za Mei Mosi mwaka 2022 huku baadhi ya wafanyakazi wakiwa na matumaini makubwa ya kupata nyongeza ya mishahara. 

 Rais Samia ni mara ya pili kuhudhuria sherehe hizo tangu aapishwe kuwa Rais ambapo kwa mwaka jana akiwa jijini Mwanza kwenye Sherehe za Mei mosi alisema hawezi kuongeza mishahara ya wafanyakazi hadi mwaka huu wa 2022 kutokana na kuwepo vikwazo mbalimbali ikiwamo janga la Corona (Uviko-19).

Pia alisema alishindwa kuongeza mishahara kutokana na hatua anazopanga kuchukua za kufuta kodi na tozo zilizokuwa zinawabughudhi Watanzania zilizosababisha kupungua kwa mapato yatokanayo na kodi.

Wafanyakazi macho na masikio yatakuwa kwake ili kufahamu atazungumza nini kuhusu maslahi na mustakabali wa ajira zao hasa kuongeza kima cha chini cha mshahara katika sekta ya umma na ile ya sekta binafsi na kupandisha madaraja wafanyakazi wa umma

Waziri wa Ulinzi azindua baraza la Wafanyakazi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 1, 2022