Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso atoa mkono wa Eid-liftri kwa watoto mayatima wanaoishi kwenye kituo Cha Ummul Yatima kilichopo Kashai Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Katika salamu zake zilizotolewa na Katibu wa Waziri Aweso Mhandisi Jafari Ally Athumani kwenye hafla ya Iftari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira BUWASA, Jafari amesema kuwa Waziri Aweso amefurahishwa na tukio lililoandaliwa na BUWASA kwa wadau wake.

Jafari ameongeza kuwa tukio hili ni la kuigwa ambalo na yeye binafsi amewiwa kushiriki kwa kutoa pesa tasilimu kiasi Cha shilingi laki mbili kwaajili ya kupeleka kituoni hapo kama mkono wa Eid-liftri.

Hata hivyo sambamba na hayo amewataka wananchi kuwa mabalozi wazuri wa Maji kwa kuhakikisha wanalipa bili za Maji huku akiwaonya watumishi wa Mamlaka kuwabambikia wananchi bili ambazo sio zao.

Sheikh Mngazija: Wachezaji wote Young Africans wapo FIT
90% ya vifo vya Uzazi hutokea katika mazingira ya Hospitali