Waziri wa zamani wa Nishati nchini Algeria, Chakib Khelil aliyehudumu kwa miaka 10 chini ya utawala wa Abdelaziz Bouteflika, amehukumiwa tena akiwa hayupo Mahakamani kifungo cha miaka 20 jela kwa ufisadi.

Mbele ya Mahakama ya Sidi M’Hamed mjini Algiers, Hakimu aliyetoa kifungo hicho pia amewahukumu Mawaziri wengine wakuu wa zamani, vifungo vya kuanzia miaka 5 hadi 10 jela kwa kosa kama hilo.

Mawaziri hao, ni Waziri wa zamani wa Kazi, Amar Ghoul, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Mohamed Bedjaoui na Wakuu wawili wa zamani wa kampuni kubwa ya umma ya hydrocarbon Sonatrach, Noureddine Bouterfa na Abdelmoumen Ould Kaddour.

Waziri wa zamani wa Nishati wa Algeria Chakib Khelil. Picha ya Wikipedia

Washitakiwa hao, walifunguliwa mashtaka kwa kufuja fedha za umma wakati wa kufunga kandarasi na makampuni ya kigeni, ambapo Mahakama imethibitisha hati ya kimataifa ya kukamatwa iliyotolewa dhidi ya Khelil.

Mapema mwaka 2013, vyombo vya sheria vya Algeria vilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Khelil kama sehemu ya uchunguzi wa malipo ya tume za siri na kampuni tanzu ya kampuni kubwa ya Italia ENI ili kupata kandarasi nchini humo, kashfa ambayo imekuwa chini ya kesi nyingine nchini Italia na Algeria.

Serikali yataka uwajibikaji udhibiti mimba, ndoa za utotoni
Aliyepanda juu ya nguzo za umeme ahojiwa na Polisi