Serikali ya Japan, imesema maporomoko ya theluji yameuwa watu 17 na kujeruhi wengine zaidi ya 90 katika muda wa siku 10 zilizopita katika eneo lililoathirika zaidi la pwani ya magharibi na jimbo la kaskazini la Hokkaido la nchi hiyo.
Taarifa zinasema, watu wengi walikutwa na mauti baada ya kuteleza wakiondoa theluji iliyoganda kwenye mapaa ya nyumba zao, au kwa kufunikwa na marundo ya theluji hiyo yaliyoporomoka kutoka juu ya nyumba.
Aidha, Mikoa kadhaa, hasa ya mji wa Oguni katika jimbo la kaskazini la Yamagata yalishuhudiwa kuwa na theluji yenye kina cha mita moja katika muda wa saa 24.
Hata hivyo, katika majimbo mengi kiasi cha theluji iliyoanguka mwaka huu ni zaidi ya mara tatu ya kiwango cha kawaida hali ambayo pia imeikumba nchi ya Marekani ambayo nayo imeondokewa na raia wake zaidi ya 50 kutokana na limbunga cha theluji.