Balozi wa kampeni ya ‘Nyumba ni Choo’ na Msanii wa muziki wa tamaduni, Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba amewaonya wamiliki wa nyumba ambao wanapangisha nyumba ambazo hazina vyoo bora na kuwataka wapangaji kutumia gharama zao nje ya kodi kufanya marekebisho ya vyoo hivyo.
Amesema kwamba wamiliki hao wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa pamoja na kuwapa adhabu kwani imekuwa tabia ya wamiliki wengi kujali kodi ya nyumba kuliko hali ya choo bora kwa wapangaji wao.
Mpoto amezungumza hayo juzi Kata ya Kiwalani Jijini Dar es salaam aliposhiriki katika kipindi cha On The Bench kinachofanywa na Dar24 Media mara baada ya kuweka kambi katika kata ya Kiwalani na kufanya majadiliano ya pamoja wananchi na maafisa Afya juu ya kwa nini mifumo ya vyoo bado ni tatizo Dar es salaam ambapo Kiwalani ni moja ya maeneo yanayokosa choo jijini Dar es salaam.
Aidha, Mpoto amewataka mafisa afya kulifanyia kazi suala hilo la wamiliki wa nyumba wanaowaza kodi kuliko choo amesema ”yaani wao choo sio muhimu, muhimu kodi”.
”Choo kitabomoka, utadumbukia, hakina mlango anajifanya halimuhusu, sheria zipo anatakiwa aripotiwe na adhabu kali inachukuliwa na ikiwezekana tutakusanya kodi zote za miezi sita tujenge choo utaratibu huo na utafanya kazi ” amesema Mpoto .
Aidha ameongezea kuwa haiwezekani umlipishe mtu kodi bila kujali afya yake.
Aidha Mpoto amesikitishwa na tabia ya watu wa Kiwalani kukosa kifaa cha kunawai ikono baada ya kutoka chooni k
Watu hawaan vyombo kwahiyo milipuko ikitokea ni nadra sana watu kupona amewataka wote waliopata elimu kuhusu choo bora kwenda kujenga choo bora na kuwahamasisha wengine kujenfga choo v=bora