Shirika la Afya Duniani WHO limesema linazitathmini ripoti za baadhi ya wagonjwa wa COVID-19 kugugundulika kuwa na virusi vya corona kwa mara nyingine baada ya vipimo vya awali kubainisha kupona ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa muongozo wa WHO mgonjwa anaweza kuruhusiwa kutoka hospitali mara baada ya kupimwa mara mbili mfululizo katika kipindi cha masaa 24.
Hata hivyo maafisa nchini Korea Kusini waliripoti kwamba wagonjwa 91, ambao walionekana kuwa salama baada ya kupimwa na baadae walipatikana na virusi vya corona katika vipimo vingine.
Mkurugenzi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa na Kinga nchini Korea Jeong Eun-kyeong amesema upo uwezekano wa virusi hivyo kupata nguvu mpya, kuliko maambukizi mapya.
Aidha Shirika la Afya duniani (WHO) limesema linachukua tahadhari zote juu ya kuwepo kwa taarifa hizo kutoka maeneo tofauti.