Wilaya ya Mbeya, imeanza kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Zuberi Homera kwa kufanya kikao na wadau wa mbolea ya ruzuku.

Akizungumza kwenye kikao hicho kilichowajumuisha Maafisa Kilimo, Ugani, Ushirika, Mawakala na Makampuni ya kuuza Mbolea, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amewataka wadau hao kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwenye eneo lake ipasavyo, ili kuondoa kasoro zote zilizojitokeza msimu uliopita.

Malisa ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Pembejeo, pia amesisitiza kuwa hataki kuona changamoto za udanganyifu wa uandikishaji na uhakiki zilizojitokeza msimu uliopita zinajitokeza tena na ndio maana ameamua kuitisha kikao hicho na watu muhimu kwenye sekta ya mbolea ya rukuzu.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 11, 2023
Museveni aijia juu Benki ya Dunia