Msanii wa muziki wa bongo fleva, Alikiba siku ya Jumanne aliachia video ya ngoma yake iliyokuwa ikisubiliwa kwa hamu na mashabiki zake inayojulikana kama ‘Hela’ jana siku ya jumatano aliamua kuindoa na leo Alhamis ngoma hiyo imerudishwa tena mtandaoni.
Leo katika kipindi cha Planet Bongo Kiba ameamua kufunguka sababu ya kuiondoa ngoma hiyo mtandaoni richa ya kuwa tayari maneno mengi yamekwishazuka yakidai kuwa ngoma hiyo iliondolewa kutokana na maoni hasi juu ya wimbo huo.
“Siku yenyewe haikuwa siku yangu ambayo napenda kurelease nyimbo, ilikuwa siku ya Jumanne so tukamwambia jamaa autoe, inatakiwa siku kama ya leo Alhamisi, ndio maana ulikuta umetoka kwenye Youtube, ila sasa hivi ukiingia utaikuta”, amesema Alikiba.
Aidha wimbo huo umeshambuliwa vikali na mashabiki na kusema ni mbaya na ni wazamani, komenti hizo ni kufuatia kwamba mashabiki wa msanii huyo wamekaa miezi kadhaa wakisubiria kibao kipya kutoka kwa msanii huyo, cha kushangaza ni kwamba ngoma aliyoamua kuiachia haijakubalika na mashabiki wake, huku mpinzani wake Diamond Platinumz akiendelea kufanya vizuri katika wimbo aliyoshirikishwa na kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Aika pamoja na Nahreel.