Kaunti ya Jiji la Nairobi, imesema inatarajia kutatupa miili 236 baada ya siku saba, ambayo imehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa muda mrefu bila kupata wahusika ambao ni ndugu zao kwa ajili ya kuwasitiri kwa taratibu za kawaida za kibinadamu.
Kupitia tangazo lililotolewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu Kaunti ya Nairobi, Fredrick Olunga amesema miili ambayo haitatambuliwa ndani ya siku saba itazikwa na Huduma ya Nairobi Metropolitan Service (NMS), na imehifadhiwa 218 wapo Jijini Nairobi na wengine 18 wako katika Hifadhi ya miili ya Mama Lucy na kusema kama itakosa wenyewe ndani ya kipindi kilichoainishwa, itatupwa rasmi.
Taarifa hiyo imesema, “Kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Umma Sura ya 242 tanzu na Kanuni ya Afya ya Umma, Wananchi wanaombwa kuitambua na kuichukua miili iliyotajwa hapa chini ndani ya siku 7 (saba), ikishindikana Kaunti ya Jiji la Nairobi itatafuta mamlaka ya kuziondoa.”
Sababu za vifo vya maiti hao, ambao baadhi inatambulika kwa sura na majina zinadaiwa kuwa ni pamoja na ajali za barabarani, mauaji, kuzama majini, kupigwa risasi, kifo cha kawaida, kifo cha ghafla, dhuluma ya kundi la watu, shoti ya umeme na kuchomwa moto.
Miili ambayo inaweza kuagwa, kutokana na kutokuwa na hitilafu ilipokelewa hivi karibuni katika vyumba hivyo vya kuhifadhia maiti katika kipindi cha kati ya mwezi Machi 2021 na Machi 2022, ikiwa imesajiliwa katika vituo mbalimbali vya Polisi.
Machi 2022, NMS ilizika miili 119 ambayo haikutambuliwa au kuchukuliwa na wanandugu ili kupunguza idadi ya maiti katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya jiji, ambapo miili 90 ilikuwa ni ya wanaume, miongoni mwao wakiwa ni waathiriwa wanne wa kujitoa muhanga na wanaume wanne wa kupigwa risasi.