Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka Mawakili wa Serikali kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na uaminifu.

Rais Samia, ameyasema hayo hii leo Septemba 29, 2022 Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa chama cha Mawakili wa Serikali, na kuzindua chama chao huku akiwataka Mawakili wote wa Serikali wakati wa kutekeleza majukumu yao watambue kuwa wamekabidhiwa dhamana kubwa ya sekta ya haki.

Amesema, upo umuhimu kwa Mawakili wa Serikali kutambua kazi ya kusimamia haki iko mikononi mwao na kwamba wananchi wengi wanahitaji msaada wa kisheria kutoka kwao.

Ameeleza kuwa katika uongozi wake anatamani kuona Mawakili hao wa Serikali wanatenda haki wakati wa kuhudumia wananchi na wawasikilize pamoja na kutatua shida zao.

Pia amewapongeza kwa kuanzisha mfumo wa Mawakili wa Serikali na kuwataka Mawakili ambao hawajajisajili katika mfumo huo kufanya hivyo mara moja.

19 wafariki kwa kunywa Pombe yenye sumu
Wito kuitambua miili 236 iliyokosa ndugu kabla ya siku saba