Wizara ya Afya ipo katika hatua za mwisho za kuanzisha mfumo wa Taifa wa uratibu na matumizi ya magari ya kubebea wagonjwa, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za dharura kwa haraka.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kupokea magari 10 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya Shilingi Bil. 1.1 kutoka Serikali ya India.
Amesema, “tuna changamoto kubwa sana kwa magari ya wagonjwa kuchelewa kufika kwa wakati, kwa hiyo tunakwenda na mfumo mmoja ambao utaingiza Ambulance zote nchini.”
Akipokea magari hayo, Waziri Ummy amewataka Madereva wake kuzingatia sheria, taratibu na matumizi sahihi ya uendeshaji gari, ikiwemo kupakia wagonjwa pekee kwani zipo taarifa kuwa baadhi ya magari hayo hubeba vitu ambavyo ni kinyume na taratibu.