Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kushirikiana na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuendelea kufunga mtandao katika Vijiji vyenye umeme, ili
kuwawezesha wanafunzi kufanya mitihani ya masomo ya Sñññayansi kwa mtandao.

Rais Samia ametoa maagizo hayo hii leo Desemba 16, 2023 wakati wa hafla ya kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Taifa – NECTA), iliyofanyika katika Ofisi za Baraza hilo.

Rais Samia akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria Maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania – NECTA, yaliofanyika katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam hii leo Desemba 16, 2023.

Aidha, Rais Samia pia amesema Serikali imefanya uwekezaji kwenye TEHAMA ambao umeimarisha utendaji wa Baraza na kuongeza matumizi ya teknolojia katika usajili wa watahiniwa, uchapaji na usahihishaji wa mitihani na uchakataji wa matokeo.

Amesema, Serikali itaendelea kuijengea uwezo NECTA na Walimu ili kuhakikisha ufundishaji, usomeshaji na utahini unafanyika kwa umahiri mkubwa
kuwawezesha watahiniwa kumudu mahitaji ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Rais Samia wakati akiwasili katika viwanja vya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwa ajili ya kushiriki kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza hilo Jijini Dar es Salaam Desemba 16, 2023.

Rais Samia pia ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na NECTA kutafuta mkakati wa kushughulikia changamoto ya udanganyifu wa mitihani na kulitaka Baraza la Mitihani kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kuendana na shabaha ya sera ya elimu hususan katika upimaji wa umahiri.

Rais Samia amesema serikali itaendelea kuimarisha utendaji wa Baraza kulingana na mazingira mapya ya kiteknolojia na kushirikiana na Baraza hilo ili lifikie malengo ya muda mrefu ya kuweka mitambo ya kisasa ya uchapaji kadri uwezo utakavyoruhusu.

Mfumo kubaini makosa Barabarani kutumiwa kikamilifu
Zaidi ya 7,000 wahitimu Chuo cha Uhasibu