Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge kuidhinisha Shilingi 15.94 trilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara hiyo makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Amesema, kiwango hicho cha fedha Shilingi 15.38 trilioni, ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 564.22 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.