Wizara ya Maliasili na Utalii imetangaza kiingilio katika maonyesho ya sabasaba kwenye banda lake yanayotarajiwa kuanza tarehe 28, june mwaka huu mpaka kilele cha maonyesho hayo tarehe 7, 7 2017.

Aidha, Wizara hiyo kupitia kitengo cha mawasiliano, imesema kuwa kiingilio katika banda lake ambalo litakuwa na maliasili mbalimbali kama wanyama, bustani na vivutio vingine itakuwa ni shilingi 1000 kwa wakubwa na watoto ni shil.500.

Hata hivyo, Wizara hiyo imewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea banda hilo ili kuweza kujionea na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu vivutio vya nchi na utalii asilia wa nchi ya Tanzania.

China yakumbwa na maafa, watu 140 hawajulikani walipo
Makamba atoa agizo kwa wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi nchini