Wizara ya Madini, hii leo Aprili 27, 2023 imetoa vipaumbele vyake kwenye mwaka wa fedha 2023/2024 kwenye lengo la kuhakikisha sekta ya madini inachangia kujenga uchumi imara na kuongeza pato la Taifa kupitia rasilimali Madini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini, Dkt. Dotto Biteko Bungeni jijini Dodoma, na kuongeza kuwa Wizara ya madini imepanga kutekeleza vipaumbele sita ikiwemo kimarisha Ukusanyaji wa Maduhuli na Kuongeza Mchango
wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa.

Vipaumbele vingine ni pamoja na kuendeleza Madini Muhimu na Madini Mkakati, kuwaendeleza na kusogeza Huduma za Ugani kwa Wachimbaji Wadogo na kuhamasisha Shughuli za uongezaji thamani Madini.

Aidha kazi kipaumbele kingine pia ni kuhamasisha uwekezaji na Biashara katika Sekta ya Madini, uanzishwaiji wa Minada na Maonesho ya Madini ya vito vya zijengea uwezo Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Madini ili
ziweze kutekeleza Majukumu yao kwa ufanisi.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Aprili 28, 2023
Watanzania waliokwama Sudan wawasili nchini salama