Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.

Wakala wa Vipimo Tanzania – WMA, umewataka Watanzania wenye mashaka na vipimo kuhakiki upya kwa ajili ya kujiridhisha ikiwemo ujazo, urefu au uzito kulingana na thamani ya fedha wanayolipa.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Viwango na Uhakiki wa Vipimo – WMA, Magesa Biyani wakati wa zoezi la kuhakiki Vipimo vya kupimia bidhaa na kutolea huduma kwa wananchi, viwandani na sehemu mbalimbali nchini.

Amesema, WMA hufanyia uhakiki wa vifaa na vitendea kazi vya huduma na bidhaa mara moja kwa mwaka, ili kuhakikisha unafanyika kwa usahihi unaotakiwa kitaifa na Kimataifa.

“zoezi hili, linazuia udanganyifu unaofanyika wakati ambapo muuzaji anahitaji kupata faida kuliko kile ambacho anampatia mteja wake hasa kipindi hiki tunapoelekea sikukuu watu hufanya udanganyifu lakini niwahakikishie tu Wananchi kwamba Vipimo vyetu ni sahihi na tunavihakiki hapa ili viweze kuwa sahihi.”

Kaze anukia Ihefu FC
Young Africans kuitumia Mtibwa Sugar kimataifa