Mlinda mlango kutoka Poland Wojciech Szczesny, anatarajia kukamilisha usajili wa kujiunga na mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC, akitokea kwa washika bunduki wa jijini London Arsenal, kwa ada ya uhamisho ya Pauni milioni  10.

Mlinda mlango huyo aliyeitumikia AS Roma kwa mkopo wa miaka miwili jana aliwasili mjini Turin kwa lengo la kufanyiwa vipimo vya afya, ikiwa ni sehemu ya kukamilisha uhamisho wake.

Szczesny, anatarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja ambao utamuwezesha kulipwa mshahara wa Pauni milioni 3.5 kwa mwaka.

Tayari Juventus wameshatoa picha ya video inayoonyesha harakati za usajili wa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 27, hali ambayo inadhihirisha wamejizatiti kukamilisha mpango huo ndani ya juma hili.

Akiwa AS Roma kwa mkopo, Szczesny, alionyesha kiwango kizuri cha kulinda milingoti miwili na kusababisha viongozi wa mabingwa wa Sirie A (Juventus FC) kumtolea macho.

Anajivuni rekodi ya kucheza michezo 14 bila kuruhusu bao tangu aliposajiliwa kwa mkopo huko Stadio Olympico.

Szczesny, alilazimika kuondoka Arsenal, kufuatia ufunyu wa nafasi ya kucheza mara kwa mara uliojitokeza, baada ya kusajiliwa kwa David Ospina na Petr Čech misimu mitatu iliyopita.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Poland, Szczesny, ameshacheza michezo 28 na matarajio yake ya kusajiliwa na Juventus yanatajwa kuwa mbadala wa mlinda mlango wa sasa  Gianluigi Buffon, ambaye yu njiani kutangaza kustaafu soka.

Mghwira amvaa Lowassa, asema kuhama chama ni ufisadi wa kisiasa
Bakwata yataka anayejiita Mtume akamatwe