Aliyekuwa Msema wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Klabu ya Yanga, Jerry Muro ameiponda Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kusema kuwa kamati hiyo ina mapungufu makubwa.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kamwe uonevu kama huo wanaoufanya kamati ya maadili ya TFF utaendelea kudidimiza mchezo mpira wa miguu hapa nchini.

“Nadhani mmeona kilichotokea kwa baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo kule walipo sasa hivi, walijua hawatajulikana ubaya ambao waikuwa wakiufanya, wakasahau kuwa siku itafika na wataumbuka,”amesema Muro.

Aidha, amesema kuwa Kamati hiyo haikutumia hekima kuweza kutoa maamuzi yaliyopelekea kufungiwa huku akiongeza kuwa mchezo wa mpira wa miguu sasa hivi unahitaji watu wenye uelewa na mchezo huo ili uweze kufika mbali zaidi.

Hata hivyo, Jerry ameushukuru uongozi wa Klabu yake ya Yanga kwa kufanya nae kazi vizuri mpaka pale mkataba wake uipomalizika,pia ameipongeza Klabu hiyo kwa kupata msemaji mpya.

Wasanii bongo chukueni hii Kwa Beiber na Dj Khaled
IGP Sirro aanza kulisuka upya Jeshi la Polisi