Wasanii wa bongo movie na bongo fleva wameingilia kati swala zima la mwanafunzi wa chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini kuuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa akiwa ndani ya daladala pindi polisi walipokuwa wakidhibiti maandamano yaliyokuwa yakifanywa na Chadema.
Jackline Wolper ambaye ni muigizaji wa Bongo Movie na mwanamitindo anayekuja juu nchini ameandika waraka akilaumu na kulaani vikali tukio hilo lililokatiza ndoto za mwanadada Akwilina.
”Nilisikia bunduki zikipigwa nikiwa ofisini kwangu kila mtu anakimbia, ilinijia picha ya Iraq na si Tanzania ile nilioizoea”. Amesema Wolper.
”Tanzania jina la nchi yetu naona si tamu tena na limeanza kuwa chungu, ile nchi yenye Hekima, Umoja na Amani inaanza kuwa nchi ya wasiwasi, mbona wachache wenye madaraka yenu mnataka kutuharibia Amani, Mtoto wa watu ambae alikuwa na ndoto zake nchini kwake ameiacha Tanzania Yake” amesema Wolper.
-
Video: Mauaji ya mwanachuo yavuruga Polisi, Wazazi watoa neno zito
-
Serikali yajitosa kugharamia mazishi ya Akwilina
-
Video: Mbowe asakwa kuhusu kifo cha mwanafunzi
Ameongezea kuwa muhusika wa tukio hilo anamuomba Mungu amlipe kwa kukatiza ndoto za binti huyo.
Amesema ”Wewe uliyefanya kitendo hiki sikuombei ufe wala uhukumiwe ila nakuombea ulipwe na Mungu kwa hiki ulichokifanya” Wolper.
Wolper amesema kuwa tukio hilo ni uonevu na kukosa maarifa, amepinga vikali utumiaji mbovu wa madaraka.
Aidha ametoa pole kwa familia zote walipoteza watu wao wa karibu, waliojeruhiwa katika harakati hizo za kisiasa.