Mabosi wa FC Barcelona wanajiandaa kumfunga zaidi kocha wao, Xavi Hernandez kwa kumuongezea mkataba mpya ambao utamuweka klabuni hapo hadi mwaka 2025.

Mabosi hao wakiongozwa na Rais wa Barcelona, Joan Laporta wanataka kumpa mkataba mrefu Xavi baada ya kukoshwa na kazi yake tangu walipomkabidhi kazi ya kuinoa timu hiyo akiwapa taji la Ligi Kuu Hispania La Liga msimu uliopita.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Hispania vimeweka wazi kuwa mkataba huo ulishaandaliwa tangu mwezi Machi mwaka huu na ilikuwa ikisubiriwa dirisha la usajili lipite kwa ajili ya kusainiwa.

Mwanampotevu amerejea nyumbani
Musonda awahidi furaha mashabiki