Klabu ya Arsenal huenda ikaonyesha maajabu ya mwaka katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili la majira ya kiangazi, ambalo litafungwa rasmi majira ya saa tano na dakika 59 kwa saa za mataifa ya Ulaya.
Gazeti la The Sun limeripoti taarifa za uwezekano wa uhamisho wa mshambuliaji kutoka nchini Chile Alexis Sanchez ambao huenda ukagharimu kiasi cha Pauni milioni 60 hadi 70.
Klabu ya Man City imedhamiria kumsajili mshambuliaji huyo wa Arsenal kabla ya dirisha la usajili kufungwa, na gazeti hilo limeripoti kuwa tayari ujumbe wa watu kadhaa umeshatua mjini London kwa ajili ya mazungumzo ya kuwashawishi The Gunners.
Mshambuliaji wa Alex Oxlade-Chamberlain tayari ameshapiga hatua ya kuondoka Arsenal, kufuatia klabu ya Liverpool kuweka dau la Pauni milioni 40 kwa ajili ya usajili wake, baada ya dili la kujiunga na Chelsea kuvunjika usiku wa kuamkia jana.
-
Diego Costa kusajiliwa kwa mkopo Hispania
-
Haji Manara afichua siri ya muonekano wa kikosi cha Simba SC
Wegine ambaye anatajwa kuondoka kabla ya dirisha la usajili ni kiungo kutoka nchini Uswiz Granit Xhaka, beki kutoka Ujerumani Shkodran Mustafi na mshambuliaji kutoka nchini Hispania Lucas Perez na beki Calum Chambers, huku Kieran Gibbs akiwa ameshathibitishwa kujiunga na West Brom kwa ada ya Pauni milioni 7.