Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus wamethibitisha kumsajili beki kutoka Ujerumani Benedikt Howedes akitokea Schalke 04.

Juventus wamethibitisha kukamilisha dili hilo, huku wakikiri kumsajili Howedes mwenye umri wa miaka 29 kwa mkopo wa muda mrefu, na kama ataonyesha uwezo wanaoutarajia watamsajili moja kwa moja itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa ya klabu hiyo ya mijini Turin imeeleza kuwa, Howedes amesajiliwa kwa ada ya Euro milioni 3.5 na atakua klabuni hapo hadi mwezi Juni mwaka 2018. Kama Juve wataafiki kumsajili moja kwa moja watatoa kiasi cha Euro milioni 13.

Hata hivyo makubalino ya usajili wa Howedes kimkataba, yanatoa nafasi kwa Juventus kumtumia kwa zaidi ya michezo 25 msimu huu endapo atakua na utimamu wa mwili, ili kuhitimisha dili la kumsajili moja kwa moja.

Howedes, alikiongoza kikosi cha Schalke 04 kama nahodha kwa kipindi cha miaka sita, anaaminiwa kuwa na uzoefu wa kutosha kucheza nafasi ya ulinzi, na usajili wake umesababishwa na hatua ya kuondoka kwa Leonardo Bonucci aliejiunga na AC Milan katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Wakati huo huo kiungo kutoka nchini Ujerumani Sami Khedira, amelazimika kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, kufuatia majeraha ya goti yanayomuandama. Khedira aliondoka kambini jana na kurejea nchini Italia kwa ajili ya matibabu.

Xhaka, Mustafi, Perez na Calum Chambers wataikacha Arsenal?
Aadhibiwa kwa kusambaza tetesi za mke wa Rais kuolewa na Dr. Dre