Mshambuliaji kutoka Burkina Fasso Yacouba Sogne amepelekwa Tunisia kwa ajili ya matibabu ya jeraha la Goti alilolipata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatani (Novemba 10) na Uongozi wa Young Africans na kusambazwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo zimeelza kuwa, Mshambuliaji huyo tayari ameshaondoka nchini kuelekea Tunisia akiambatana na daktari wa viungo Youssef Mohamed.
Kutokana na matibabu ambayo atafanyiwa nchini Tunisia, huenda Yacouba akawa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu kutokana na ukubwa wa jeraha lake.
Yacouba anaelekea kwenye miezi sita ya mwisho ya mkataba wake ndani ya Young Africans, lakini kocha Nabi bado anamuhitaji kikosini na tayari Uongozi upo kwenye mazungumzo ya kumpa mkataba mpya.