Muwekezaji wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Mohamed Dewji ‘Mo’ amemkaribisha Kocha Mpya wa klabu hiyo Franco Pablo Martin nchini Tanzania.

Kocha Franco aliwasili jijini Dar es salaam leo Jumatano (Novemba 10) na kupokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Mratibu wa Simba SC Abbas Haji.

‘Mo’ amemkaribisha Kocha huyo kutoka nchini Hispania kwa kuandika ujumbe maridhawa katika kurasa za Mitandao yake ya kijamii.

“Nina furaha kumkaribisha ndani ya familia ya Simba, Kocha Pablo Franco, ambae alikua kocha msaidizi wa zamani wa Real Madrid. Karibu Tanzania, na Karibu Simba!” ameandika ‘Mo’

Simba SC ilifungua Dirisha la kusaka Kocha Mpya baada ya kuachana na Didier Gomes mwishoni mwa mwezi Oktoba, kufuatia kocha huyo kutoka nchini Ufaransa kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba Ilikwama kwenye Michuano hiyo, kufuatia kufungwa maboa 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salam, huku ikitangulia kushinda ugenini mjini Gaborone mabao 2-0.

Taifa Stars kuifuata Madagascar kwa Air Bus
Yacouba Sogne apelekwa Tunisia