Hivi karibuni Meneja wa kundi kutoka mkubwa na wanawe Said Fella ”yamoto band” alisikika katika kipindi cha E news cha Eatv alisikika akisema Rubby kutokuonekana kwenye Video ya SU aliyoshirikishwa na Yamoto Band ni kutokana na Stress.

Hata hivyo mwanamuziki huyo aliyejulikana kupitia tamasha la supa nyota Diva la Serengeti Fiesta ameibuka na kueleza  masikitiko yake juu ya kutoshirikishwa katika video hiyo ambayo inasumbua kwa sasa mjini.

“Nimeumia sana maana audio ile tumefanya muda mrefu na waliweza kusubiri mpaka tukakamilisha iweje kwenye video washindwe kunisubiri, maana hii kazi tunasaidiana,” alisema Ruby.

Rubby amekiambia kipindi cha Planet bongo cha East afrika radio kuwa wakati yamoto band wanashooyt  hiyo video yeye alikuwa na mambo mengine hivyo akawambia wamsubiri amalize ili aungane nao.

”Inawezekana hawakuona umuhimu wangu ndio maana walishindwa kunisubiri” alisema Rubby.

Suala hili bado linamkanganuiko kwa mashabiki hivyo bado tunaendelea kutafuta ukweli ni upi?

Joseph Marius Omog Asaini Miaka Miwili Simba
Bakari Shime: Hakutokua Na Mabadiliko Ya Kikosi