Baada ya kutokupata mafanikio msimu wa 2018/2019 uongozi wa kikosi cha Yanga sasa unaonekana hautaki yaliyo tokea awali ya jirudie tena.

Kwa kudhihirisha hilo Yanga tayari imenasa saini ya beki kutoka nchini Ghana anaye fahamika kwa jina la Lamine Moro ambaye ataitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka miwili.

Sasa himaya ya ulinzi ya Yanga inatarajiwa kuongezwa nguvu na  Moro.

Kipindi cha nyuma Moro aliwahi kuja nchini kwenye michuano ya sportpesa na kufanyiwa majaribio na klabu ya Simba ambayo ni wapinzani wa wana hao wa Jangwani.

Baada ya kumalizana na kiungo Patrick Sibomana kutoka Rwanda, Yanga imezidi kuboresha kikosi chake kutokana na wachezaji wengi kumaliza mikataba yao msimu huu uliomalizika.

Sibomana, Moro wametanguliwa, Papy Tshishimbi na Issa Bigrimana ambao tayari wameshasaini kuitumikia timu hiyo.

Usajili huu umekuwa pendekezo la Kocha Mwinyi Zahera ambaye amekabidhiwa majukumu ya kuhakikisha anapendekeza wachezaji wanaopaswa kusajiliwa.

 

 

 

Fainali ya UEFA yatoa shavu kwa Polisi
UVCCM Iringa waaswa kuwatetea wanachama