Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga imeingia mkataba miaka 3 wa bilioni mbili na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo Macron.
Mara baada ya kusaini mkataba huo Yanga imesema itaanza kuwashughulikia kisheria wanaouza jezi za klabu hiyo kiholela bila makubaliano yeyote.
Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa kufuatia mkataba uliosainiwa kwenye ofisi za makao makuu ya klabu hiyo, ambapo amesema kuwa Yanga itawapa Macron haki zote za utengenrzaji na usambazaji wa jezi zao.
Aidha kupitia makubaliano hayo nembo ya kampuni ya Macron itaanza kuonekana kwenye jezi za Yanga SC, hivyo uuzaji kiolela wa jezi hizo umepigwa marufuku kwani mwenye haki ya kufanya hivyo sasa yupo.
Pia Mkwasa amewakaribisha wawekezaji zaidi ndani ya klabu hiyo.
Naye Mkurugenezi mtendaji wa Macron hapa Tanzania, Suleiman Karim amewahakikishia wana Yanga kupata faida kupitia mauzo ya jezi orijino za klabu.
Kampuni ya Macron inafanya kazi katika nchi zaidi ya 16 duniani zikiwemo England, Italia na Ufaransa. Hivi karibuni kampuni hiyo iliingia mkatata wa miaka 2 na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wenye thamani ya milion 800.