Kumekuwa na taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na Klabu ya Simba kumtoa Haji Manara kwenye nafasi yake ya ofisa Habari kwa sababu ambazo hazikufahamika mara moja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amelizungumzia hilo kwa kueleza kuwa hakuna kitu kama hicho wale wanaomchukia na kusambaza taarifa ambazo siyo za kweli.

Manara ameweka picha ya mtu aliyesambaza taarifa hizo kupitia Instagram kisha ameandika maelezo haya.

“Kuna mpumb** mmoja aliyejitambulisha kama Mwenyekiti wa Group la Yanga WhatsApp supporters makao makuu, anazusha mitandaoni kuwa nimeondoka Simba…hahahahaha sitakaa milele pale kama yeye na wapumb** wenzie watavyoondoka huko walipo, lakini kwa sasa mm ndiyo msemaji wa Big brand ya nch….. , unavyozidi kunichukia ndiyo unazidi kunisogeza…. Kwa mnaoniogopa wote niwaambie NA BAO.”

Alikiba ashinda tuzo ya kijana mwenye ushawishi Afrika 2017
Sugu: Najisikia kama Nyerere wakati wa Ukoloni au Mandela wakati wa Ukaburu