Msanii wa nyimbo za Bongo Fleva, Mfalme Ali Kiba anayefanya kazi zake chini ya lebo ya Rockstar 4000 na Sony Music Entertainment, ambaye pia anafanya vizuri katika sanaa hiyo ya muziki na hivi karibuni ametamba sana na kibao chake cha ‘’Seduce me’’ kilichovunja rekodi kuliko nyimbo zake zote kwa kusikilizwa na kushabikiwa na watu wengi.

Alikiba amejishindia tuzo ya kuwa kijana mwenye ushawishi mkubwa Afrika kwa mwaka 2017 ambapo ameshinda tuzo inayoenda kwa jina la 100 Most Influencial Youth Africans inayotolewa na Africa Youth Awards ikiwa ni namna mojawapo ya kumpongeza kwa jitihada anazozifanya katika fani yake na uhamasishaji wa vijana katika kusaka maendeleo.

Ikumbukwe kuwa aliyekuwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikiwete anatambua mchango wa Ali Kiba katika sanaa ya Muziki wa Tanzania na anaheshimu mchango huo kwa kiasi kikubwa sana .

Kwa Tanzania tuzo hiyo imekuwa ikiwaniwa na wasanii wengi na wakubwa akiwemo, Jokate Mwagelo, Idriss Sultan, Ambwene Yessaya, Diamond Platinumz na wengine wengi walionesha juhudi za kimaendeleo katika mwaka 2017.

Alikiba kupitia ukurasa wake instagram ametoa shukrani kwa wote waliona mchango wake na kumpigia kura na kupata tuzo hiyo, ameandika ‘’Nashukuru Sana’’

Zitto agonga mwamba Kigoma Mjini
Manara awajibu waliomzushia kutimuliwa Simba