Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama  ‘Sugu’ na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga mapema leo hii wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Wawili hao wamefikishwa mahakamani hapo wakituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi katika hotuba zao walizotoa katika Mkutano wa Hadhara  uliofanyika tarehe 30 Disemba, 2017 katika kiwanja cha Shule ya msingi Mwenge iliyopo katika Kata ya Ruanda jijini Mbeya.

Ambapo Sugu kupitia mkasa huo amewaasa wanamabadiliko kutoogopa kwani hata yeye haogopi.

“Polisi wameniita wanipeleke mahakamani kwa wanachodai ni ‘Uchochezi, Najisikia kama Nyerere wakati wa Ukoloni au Mandela wakati wa Ukaburu, Siogopi na msiogope’’ amesema J. Mbilinyi.

Ambapo wabunge hao wawili wamepelekwa mahabusu baada ya mahakama ya Mbeya kuwanyima dhamana na kuamuru wapelekwe rumande mpaka tarehe 19 Januari 2018 ambapo uamuzi utatolewa juu ya dhamana iliyoombwa kwani watuhumiwa hao walikana mashtaka yanayowakabili.

 

Manara awajibu waliomzushia kutimuliwa Simba
Ahukumiwa kwa kubaka mbuzi wawili