Imefahamika kuwa Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans kitaondoka Dar es salaam kesho Alhamis (Februari 23), majira ya alfajiri kuelekea Mali.

Taarifa imeeleza kuwa safari ya Young Africans itaanza saa 10:25 alfajiri kwa shirika la ndege la Ethiopia, tayari kwa mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya AS Real Bamako, utakaopigwa Jumapili (Februari 26) mjini Bamako.

Msafara wa kikosi cha Young Africans utapitia Ethiopia kwa mapumziko mafupi, kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Mali saa 10:40 asubuhi na kuingia Bamako saa 8:40 mchana.

Mchezo wa Young Africans dhidi ya AS Real Bamako utachezeshwa na Mwamuzi Joshua Bondo kutoka Botswana, katika Uwanja wa Machi 26.

DART waomba radhi ajali Kisutu
Makamu wa Rais mgeni rasmi kongamano la uwekezaji