Uongozi wa Young Africans umesisitiza kuzihitaji alama tatu kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Liti mkoani Singida kesho Alhamisi (Mei 04).

Tayari kikosi cha Young Africans kimeshawasili mjini Singida kwa ajili ya mchezo huo, ambao umepangwa kuanza mishale ya saa kumi jioni.

Afisa Habari wa Young Africans Ally Shaban Kamwe amesema wanatambua uimara wa wapinzani wao hivyo watawakabili kwa tahadhari kupata ili kukamilisha lengo la kupata alama tatu za mchezo huo.

“Kila mchezo kwetu ni muhimu kupata ushindi, tunatambua wapinzani wetu wanahitaji kushinda tunawaheshimu lakini nasi tunahitaji alama tatu pia.”

“Benchi la ufundi na wachezaji kiujumla wapo tayari kwa mchezo na tunaamini mbinu zitaleta matokeo mazuri kikubwa ni mashabiki kujitokeza na kushangilia timu yao bila kuchoka,” amesema Kamwe.

Young Africans ina alama 68 ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 63 zote zikicheza michezo 26.

Katika mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza dhidi ya Singida Big Stars uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Young Africans ilichomoza na ushindi wa 4-1.

Marumo Gallants yaandaliwa mkakati mzito Dar
GGML kampuni kinara uzingatiaji wa malengo SDGs