Kikosi Cha Young Africans kimeanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam, kikitokea Mkoani Kigoma, ambako jana Jumatano (Mei 04) kilicheza mchezo wa Mzunguuko wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Lake Tanganyika ulishuhudia miamba hiyo ikimaliza dakika 90 bila kufungana.
Young Africans inarejea jijini Dar es salaam kuanza maandalizi ya mchezo ujao ambao utawakutanisha dhidi ya Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’.
Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili (Mei 09), huku Young Africans ikiendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 56.
Mchezo wa Duru la kwanza uliozikutanisha timu hizo Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa, Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.