Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans wamewatumia salamu Mabingwa watetezi Simba SC na kuwataka wasahau kuwatoa kileeni mwa msimamo kwa sasa.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa tofauti ya alama 5, huku ikiwa imecheza michezo 14, tofauti na Simba SC iliyocheza michezo 15 hadi sasa.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Young Africans Hassan Bumbuli amesema alama 5 zinazowafanya kuwa kileleni, zinawapa hali ya kujiamini kuwa na matumaini makubwa ya kufikia malengo yao ya ubingwa.

“Tunaongoza ligi ipo wazi na tumewaacha wapinzani wetu kwa tofauti ya pointi tano, hizo sio za kubeza zinatupa nguvu ya kuweza kusaka ubingwa wa ligi na tunahitaji kuweza kutwaa kwa kuwa tumejipanga.

“Wachezaji wapo tayari na benchi la ufundi linaendelea kuwapa mbinu wachezaji, mapumziko yamekwisha kila mmoja kwa sasa yupo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu ujao na haitakuwa kazi rahisi kupata ushindi lakini tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo,” amesema Bumbuli.

Young Africans ipo kileleni kwa kumiliki alama 36, huku Simba SC inayoshika nafasi ya pili kwa kufikisha alama 31 baada ya kucheza michezo 15.

Young Africans itacheza mchezo wake wa 15 dhidi ya Mtibwa Sugar Februari 23, Uwanja wa Manungu, Mkoani Morogoro.

Vaeni barakoa wakati wa kushiriki mapenzi
Wamachinga watengewa bil. 200 kwa ajili a mkopo