Benki ya NMB na Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) wameingia makubaliano kuanzisha bima ya moto na mafuriko ili kuwapa uhakika wa usalama wa mali zao.

Benki hiyo pia imetenga Sh. bilioni 200 kwa ajili ya mkopo kwa machinga ambapo atakuwa na uwezo wa kukopa kuanzia Sh. 500,000 hadi Sh. milioni 5.

Akizungumza wakati wa kuweka saini makubaliano hayo yaliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Filbert Mponzi, amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na wajasiriamali wa viwango vyote nchini hususani kulinda mali zao.

Amesema kuwa benki hiyo inathamini juhudi za wajasiriamali wadogo (SME’s) na kwa kudhihirisha hilo benki hiyo imejikita zaidi kuhakikisha shughuli zao zinakua.

Young Africans yaitambia Simba SC
Simba SC yawashukuru mashabiki