Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Young Africans Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameipa nafasi kubwa klabu hiyo kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kwa kuichapa Rivewrs United ya Nigeria.

Young Africans itaanzia ugenini Nigeria kucheza mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa hatua hiyo April 23, kabla ya kumalizia nyumbani jijini Dar es salaam katika Uwanja wa Benjamin Mkapa April 30.

Kocha Micho ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Uganda The Cranes, amesema kwa uzoefu alionao kwa timu za Afrika anaiona Young Africans kuwa na nafasi kubwa na uwezekanao wa kufuzu kwenda nusu fainali kwa asilimia 75 kutokana na mabadiliko makubwa iliyoyafanya kikosini.

Kocha huyo aliyeinoa Young Africans mwaka 2007, amesema kitendo cha Klabu hiyo kuwa na Mshambuliaji Fiston Mayele aliye kinara wa mabao Ligi Kuu akiwa na 16 na mwenye mwendelezo mzuri wa kufunga, anaamini kitaendelea kuibeba timu hiyo sambamba na nyota wengine ambao wameipigania timu hiyo tangu ilipokuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nimeifundisha Young Africans. Kuna mabadiliko makubwa ya kiuchezaji na hata aina ya wachezaji. Niseme mechi na Rivers inatabirika kwani sasa hivi Young Africans ina kiungo mzuri kama Khalid Aucho ambaye anaichezea timu ya taifa ya Uganda, Mayele na wengine wanaoweza kuipigania na kuivusha,” amesema.

Mshindi wa Jumla kati ya Young Africans na Rivers United atakutana na mshindi wa Jumla wa mchezo kati ya Pyramids ya Misri na Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

Air Tanzania yakiri kupitia changamoto
Namna Rais Samia alivyofukia shimo la Trilioni 1.5