Klabu ya Young Africans leo Jumatano (Januari 05) imeingia makubaliano na Kampuni za KILINET na N-Cards kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazotumiwa na Wanachama wa klabu hiyo.
Hiyo ni sehemu ya hatua za awali kwenye mfumo mpya wa uendeshaji ambapo kadi moja itauzwa shilingi 29,000.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha amesema kuwa ni hatua kubwa na anaamini kwamba Kilinet italeta utatuzi wa kidigitali kwa klabu.
“Kilinet inaleta utatuzi wa kidigitali kwa klabu na N-Cards wanaileta kadi ynyewe. Hatua hii ni kubwa na itaweza kurahisisha kujua idadi ya wanachama ambao wapo pamoja na kuweza kurahisisha masuala ya malipo ya kadi,”.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kilinet, Mohamed Saleh amesema:”Leo imekuwa siku ya kihistoria na sasa hivi klabu ya Yanga inaenda katika mabadiliko ya kidigitali na Kilinet tumepata fursa ya kufanya kazi na Yanga kuleta teknolojia za kisasa kwa ajili ya kuliwezesha ili jambo kufanyika kikamilifu.
“Jukumu la Kilinet ni kuangalia na kuzifanyia kazi michakato na mikakati ya Yanga kwa kutumia teknolojia za kisasa”.