Young Dee aka Paka Rapa ameitetea ngoma yake ya ‘Bongo Bahati Mbaya’ kufuatia tuhuma kuwa inahamasisha Watanzania kutokuwa wazalendo na kutamani wangezaliwa ughaibuni.
Rapa huyo amekana tuhuma hizo akiwatupia mpira watu ambao amedai wanatafsiri vibaya mashairi ya wimbo huo ambao ndani ya muda mfupi ulikuwa ‘habari kubwa ya burudani’.
Alisema lengo lake la kuipika ngoma hiyo lilikuwa kuionesha Serikali vitu ambavyo wananchi wanapenda na maisha yanayowavuta wengi na sio vinginevyo. Alisema kuwa aliiandika ngoma hiyo kutokana na mazingira ya maisha anayoishi na maisha ambayo vijana wengi wanatamani kuishi.
“Mimi nadhani ni ujumbe kwa serikali kwamba vijana wanapenda kuishi kwenye nchi inayofanana na Ulaya, kuanzia kwenye miundombinu… Watu wakiumwa wanatibiwa hapa hapa,” Young Dee ameiambia XXL ya Clouds FM.
- Video: Lissu awageukia usalama wa taifa, amtaka IGP Sirro kupambana na wahalifu
- Fid Q Kuwalipa mashabiki fadhila mara mbili
Kadhalika, Young Dee ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa hatua inazochukua kuwaletea wananchi maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu.