Kiongozi wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA), Raila Odinga amefungua kesi ya kupinga ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti.

Mawakili wa muungano huo wamewasilisha nyaraka za kesi hiyo na ushahidi katika Mahakama Kuu nchini Kenya saa moja kabla ya muda uliokuwa umepangwa kumalizika

Aidha, mgombea urais wa chama hicho na waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga alikuwa ameapa kutopinga matokeo ya urais mahakamani kabla ya uchaguzi kufanyika na baada ya matokeo kutangazwa, lakini baadaye alibadili msimamo wake huo na kuamua kwenda kupinga matokeo hayo.

“Tumeamua kwenda mahakamani kufichua jinsi uongozi wa kompyuta ulivyofanikishwa kuiba kura zetu, Hawa ni viongozi wa kompyuta, walifanya njama zote za kuiba kura kwaajili ya kusaidia Uhuru Kenyatta kushinda,”amesema Odinga

Hata hivyo, Odinga bado amesimamia msimamo wake  kuwa mitambo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi IEBC ilidukuliwa na matokeo kuvurugwa hivyo kumsaidia Kenyatta kushinda katika uchaguzi huo.

Young Dee aitetea ‘Bongo Bahati Mbaya’ dhidi ya tuhuma...
Fid Q Kuwalipa mashabiki fadhila mara mbili