Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema hawana wasiwasi na mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana wiki moja ijayo huko Lusaka, Zambia.

Mkwasa amesema hayo baada ya wapinzani wao kutotoa taarifa za ujio zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya pambano hilo.

“Niseme tu kuwa, hadi hivi sasa uongozi wa Yanga hatujapata taarifa zozote kutoka kwa wapinzani wetu kuhusiana na tarehe ya kutua nchini, labda kitu kikubwa nitakachokisema ni kuwa sisi tumejiandaa kupata ushindi kwenye mechi hii ya nyumbani,” Mkwasa anakaririwa.

Amesema huo usiri wanaoufanya Zanaco hawauhofii, kwani timu yao ina wachezaji na makocha, George Lwandamina na Noel Mwandila waliokuwa wanaifundisha Zesco inayoshiriki katika Ligi Kuu ya Zambia.

 

Bodi ya utalii kuitangaza Tanzania kimataifa
Prof. Ndalichako atoa msaada Taasisi ya Saratani