Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 4.5 milioni katika Taasisi ya Satarani ya Ocean Road.
Misaada hiyo iliyokabidhiwa ni pamoja na kanga, sabuni za kuogea na kufulia, dawa za meno, juisi, maji ya kunywa, pampers na mabeseni.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Prof. Ndalichako amesema katika kusherehekea siku ya wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) waliadhimia kuwatembelea wanawake wanaotibiwa saratani.
“Tunatambua kwamba wana mahitaji pia, kama ilivyo wanawake ndiyo nguzo ya maendeleo kwa hiyo anavyougua kwa muda mfupi familia hutetereka, tumekuja hapa na vifaa mbalimbali ambavyo tunaamini hawa wagonjwa wanavihitaji,” amesema Prof. Ndalichako.

Zanaco FC Yaficha Ujio Wake, Mkwasa aisemea Yanga
Magazeti ya Tanzania leo Machi 9, 2017